GET /api/v0.1/hansard/entries/646423/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 646423,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/646423/?format=api",
    "text_counter": 304,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Katika mradi wa LAPSSET, imezungumzwa kwamba Berth 1, 2 na 3 zimetengenezwa. Katika Bandari ya Mombasa, Berth 19 pia imetengenezwa. Rais aliongea mambo yaya haya mwaka jana na mwaka huu pia amezungumza zaidi. Mpango mzima wa ajira kwa watoto na watu wetu katika sehemu hizo za Bandari bado haujazungumziwa. Tukiangalia zaidi, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kenya Ports Authority (KPA ), Catherine Muturi, yuko pale mpaka saa hii lakini hajathibitishwa kamili kama Mkurugenzi Mkuu wa Bandari zetu. Hatuwezi kama binadamu ama viongozi kuzungumza yote mabaya. Kama Upinzani, yale mabaya tutasema ni mabaya na yale mazuri tutasema ni mazuri. Ninapongeza Serikali hii kwa kuweka stima katika shule nyingi hapa nchini. Kwa mfano, kule Mombasa ninakotoka, kuna taa za barabarani katika maeneo mengi na uhalifu umeshuka chini. Hili tumeliona ni jambo nzuri. Ni muhimi tupongeze Serikali kwa jambo kama hili. Hatuwezi kupinga kila kitu. La mwisho kabisa, mabenki yanaanguka. Ni lazima Serikali hii iangalie vile Imperial Bank, Dubai Bank na Chase Bank zilivyoanguka. Wananchi wadogo wadogo wanaofanya kazi na kuweka pesa zao pale sasa hawana faida ya kuendelea mbele katika maisha yao kwa sababu wanatarajia kupata mikopo. Kwa hayo machache, ninakushukuru Mhe. Spika kwa kunipa nafasi hii kuchangia Hotuba ya Rais. Asante sana."
}