GET /api/v0.1/hansard/entries/646958/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 646958,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/646958/?format=api",
    "text_counter": 227,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kusisimua misuli. Serikali yetu imesukumwa hadi pempeni. Tumeambiwa tusipopitisha Mswada huu kwa haraka, wanariadha wetu hawataruhusiwa kushiriki katika mashindano ya kimataifa. Ni jambo la aibu kuona taifa letu linalosifika sana katika michezo ulimwenguni likishurutishwa kuupitishe Mswada kama huu. Huu ni mfano mbaya kwa sababu tunaonekana kama tulikuwa tukiunga mkono mambo haya. Si lazima tushurutishwe kupitisha Miswada hapa. Tungeshughulikia Mswada huu hapo awali bila kushurutishwa na shirika lolote. Ijapokuwa naunga mkono Mswada huu, umechelewa sana kuwasilishwa hapa. Wiki iliopita, tulishuhudia wachezaji wetu wa kandanda wakitolewa katika mashindano ya Afrika kwa sababu ya udanganyifu na mazoezi duni. Lazima tuwe na sheria kali zitakazopinga hatua kama udanganyifu katika mambo ya michezo. Ghadhabu iliowekwa katika Kipengee cha Sita cha Mswada huu lazima izingatiwe kufa kupona. Kipengee cha 42 kinasema kwamba ikiwa mtu amekataa---"
}