GET /api/v0.1/hansard/entries/648165/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 648165,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/648165/?format=api",
"text_counter": 350,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia hii nafasi. Nitachukua muda mfupi. Naunga mkono Mswada huu kwa sababu unapatia wanawake wa hii nchi nafasi ya kujumuika na viongozi wengine katika kufanya maamuzi ya maendeleo ya nchi hii. Tunakumbuka Rais Obama wa Marekani alipokuja nchini alitoa hotuba nzuri sana wa kuunga sheria kama hii mkono. Alitukumbusha kuwa tukiacha wanawake nyuma ni kama timu ya mpira inayochezesha wachezaji nusu. Kutengeneza sheria ili wanawake waongezeke hapa Bungeni ni kitu ambacho kitatufanya sisi kama nchi tusonge mbele kwa pamoja. Kitu kingine, utaona katika dini, mila zetu na maneno ya wahenga, kuna maneno ya kuonyesha kuwa wanawake ni kiungo muhimu katika jamii. Kwa mfano, katika Dini ya Kiislamu, Mtume Mohammed (Rehema na amani ziwe juu yake) alisema kuwa mama ni madrasa ama shule. Kwa hivyo, ukimpatia mwamake nafasi ya kuongeza elimu na kuchangia katika uongozi, basi ile familia itaimarika na jamii kwa ujumla itanawiri. Pamoja na hiyo, kuna msemo wa Kiingereza unaosema kuwa ukielimisha mwamke mmoja ni kama umeelimisha jamii nzima. Hii inaonyesha umuhimu wa wanawake katika uongozi. Tukiwaacha nyuma tunaacha Kenya nyuma na tutashindwa na nchi zingine. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}