GET /api/v0.1/hansard/entries/648166/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 648166,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/648166/?format=api",
    "text_counter": 351,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Kitu kizuri kwa huu Mswada ni kusema kuwa wakati wowote kusiwe na zaidi ya theluthi mbili ya jinsia moja katika Bunge la Kitaifa au Seneti. Hii inahakikisha kuwa hakutakuwa wakati ambapo kuna wanaume au wanawake watupu Bungeni kama ilivyokuwa siku zilizopita katika nchi hii. Kitu ambacho nafurahia pia ni kuwa si wanawake tu wamepewa nafasi; ni kwa sababu hivi sasa walioachwa nyuma ni wanawake na sio wanaume. Haitupi tu nafasi ya kuteuliwa kama wanawake watakaochaguliwa, lakini pia imetuwekea kiwango cha miaka 20 kutoka sasa. Tunapewa miaka 20 wanawake wateuliwe na kupata uzoefu wa uongozi wa Bunge ili baada ya hapo wafuatilize vile viti vingine vya kuchaguliwa. Kuna mifano michache tu ya haraka ya uzuri wa wanawake kuja Bungeni. Kuna sheria za kuzuia watu kudhulumiwa kimapenzi ambazo zimeletwa hapa na Mbunge wa kitambo ambaye sasa ni Jaji wa Mahaka ya Juu ya Kenya. Kuna sheria zinazopinga vita vya manyumbani pia zilipitishwa kwa sababu ya msukumo wa wanawake. Kuna sheria zingine ambazo, kwa mfano, zimeondoa ushuru kwenye visodo ambavyo wanawake hutumia wakiwa kwenye hada zao za mwezi. Hizo sheria zimepitishwa kwa sababu ya kuwa na wanawake Bungeni. Si masuala hayo peke yake. Ni muhimu kupata maoni ya wanawake katika sheria za nchi hii ili tusonge mbele. Hii ni kwa sababu idadi ya wanaume kwa wanawake ni asilimia sawa. Nawaomba Wabunge wenzangu wahakikishe kuwa vijana wa kike wako katika orodha ya watakaoteuliwa. Isiwe ni wanawake watu wazima pekee ambao watateuliwa. Kwa hayo machache, shukrani Naibu Spika wa Muda."
}