GET /api/v0.1/hansard/entries/648184/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 648184,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/648184/?format=api",
    "text_counter": 369,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii kuunga mkono Mswada huu unaohusu akina mama. Vile wenzangu wamezungumza ni kweli. Akina mama ndio wanaofanya kazi yote. Kila kazi katika pembe zote za Kenya zinahusu akina mama. Naunga mkono Mswada huu ambao umeletwa Bungeni. Uwezo wa kuwa kiongozi unatoka kwa Mungu. Hatujui ni kwa nini kina mama wanakatazwa kuwa viongozi. Katika Jimbo la Samburu, mama alikuwa amewekwa nyumbani kuchunga nyumba na kufanya kazi zote za nyumbani. Kenya nzima, kuna wazee ambao wanajijengea nyumba. Kwetu mama huwa anajijengea nyumba. Kama huna nyumba, bwana hataishi nawe. Lazima ujenge nyumba hiyo ili mzee huyo aje. Nilipigania kuwa kiongozi kwa sababu nilipendezwa sana kuwa kiongozi. Ningeenda kwa mkutano ya Wasamburu na ningefukuzwa kama mbwa. Wangeuliza: Mwanamke huyu anataka nini? Nashukuru Mungu kwa sababu wakati walinipatia nafasi ya kuwa kiongozi, walijua kuwa mwanamke anaweza kuwa kiongozi bora hata kumshinda mwanamume."
}