GET /api/v0.1/hansard/entries/648204/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 648204,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/648204/?format=api",
"text_counter": 389,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Katana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 691,
"legal_name": "Aisha Jumwa Katana",
"slug": "aisha-jumwa-katana"
},
"content": "Nawapa changamoto wenzangu ambao tumechaguliwa katika viti hivi maalum ya kwamba tumestawi ya kutosha. Tunaweza kuingia katika nyanja hii kung’ang’ana na wanaume. Nataka niwapongeze akina Millie Odhiambo, Cecily Mbarire, Dr. Laboso na Shebesh waliokuja hapa kama wateuliwa. Lakini waliporudi kila mtu aliingia katika eneo bunge na tumeona wamerudi hapa. Kwa hivyo wale mama 47, badala ya kungoja na kuzizuilia zile nafasi kwa wanawake wengine katika jamii na katika taifa hili, tujitoe na tutafute kwa sababu vile anafanya mwanaume hapa Bungeni sisi tunaweza kufanya zaidi. Tumewashinda sana. Si Mary Wambui peke yake vile, Mhe. Chris amesema. Wako wengi ambao wamewashinda hawa ndugu zetu katika rasilimali."
}