GET /api/v0.1/hansard/entries/648797/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 648797,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/648797/?format=api",
    "text_counter": 523,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Asante, Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninaomba niliunge mkono pendekezo la Mhe. Mwadime. Ni jambo la kawaida mara nyingi kuona watu wamepewa hifadhi na wenzao katika makao ama shamba ambalo ni la wenyeji kulingana na sheria. Baadaye, wanaanza kutumia hiyo nafasi vibaya. Mara nyingi huwa ni shida kuwaondoa watu hao. Kwa hivyo, pendekezo la Mhe. Mwadime linaweka mkazo, mbinu na njia ambazo zitatumiwa wakati mtu amekuwa ni wa shida na hawezi kukubalika kwa sababu ya unyonge ama vile anavyotumia ardhi hiyo bila kufuata mapendekezo yaliyokubaliwa."
}