GET /api/v0.1/hansard/entries/648867/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 648867,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/648867/?format=api",
"text_counter": 593,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mheshimiwa Naibu Mwenyekiti wa Muda, laiti sheria hizi zingekuwa katika lugha ya Kiswahili mungeelewa kikamilifu kile ambacho Mheshimiwa Mwadime anamaanisha. Lakini kwa sababu tunazitunga sheria hizi kwa lugha ya Kimombo, Mheshimiwa Mwadime anapotumia neno “ traditional ” anamaanisha wenyeji. Tukianza kuingilia suala la wenyeji ndipo haya masuala mengine yanaingilia. Kuna utata kuwa wenyeji ni kina nani na waliokuja ni kina nani? Haki zao zikoje? Je, waliokuja wakiwa wengi watawanyima wenyeji haki zao? Natumai haya ndio masuala ambayo Mswada huu ulitakiwa ufafanue, ueleze na uweke baana wazi wazi usawa uko wapi. Lakini kwa sababu tunazitunga sheria hizi tukitumia lugha ya Kiingereza, inakuwa shida kwa wenzetu kuona kuwa Mheshimiwa Mwadime analenga wenyeji wa taifa ili wasipokonywe ardhi ambayo wanaitumia. Naomba tumuelewe Mheshimiwa Mwadime kikamilifu."
}