GET /api/v0.1/hansard/entries/649010/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 649010,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/649010/?format=api",
"text_counter": 736,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Asante sana Mhe. Naibu Mwenyekiti wa Muda. Ninapinga sana mabadiliko haya kwa sababu tunajua kuwa Mswada wa mambo ya mashamba haukuzungumzia Mswada wa kipekee katika mambo ya dhuluma za kihistoria, haswa mambo ya mashamba. Kule kwetu Pwani, zile manuspaa ambazo zilikuwa pale zilifanya madhambi mengi sana kuhusu ardhi za jamii. Ardhi nyingi za jamii zilichukuliwa. Nyingine ziliambiwa ni wakfu lakini zinatumiwa na watu binafsi. Kwa hivyo, kuweka mabadiliko haya kunamaanisha kuwa walioibiwa ardhi zao hawatapata haki. Kwa hivyo, ninaunga mkono ibaki vile vile ilivyokuwa imewekwa awali katika Mswada huu ndio tuupitishe lakini mabadiliko haya yataleta cheche kubwa sana ambazo hatuzitaki katika nchi yetu."
}