GET /api/v0.1/hansard/entries/649335/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 649335,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/649335/?format=api",
    "text_counter": 1061,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, nami pia nataka kuchukua fursa hii kuwapongeza Mheshimiwa Alex Mwiru pamoja na timu yake ya Kamati ya Ardhi ambao wamefanya kazi nzuri sana na haswa kuweka masaa mengi kuweza kutekeleza kazi hii. Vile vile, ningependa kuwapongeza ndugu zangu wote Wabunge kwa ujumla na haswa Wabunge kutoka Pwani ambao pia, wamelivalia njuga jambo hili kuhakikisha kuwa wameweza kufanya kazi kwa pamoja na kufikia uwiano na kukubaliana kuwa masuala haya ni mazuri. Tuweze kuyaangalia tukiwa pamoja na tukubaliane. Tunafahamu ya kwamba suala la ardhi ni suala ambalo limekuwa kidonda sugu hapa nchini na haswa maeneo yetu ya Pwani ambapo suala kubwa ambalo limekuwa likikera kila mtu ni suala la mashamba. Ningetoa mfano tu. Katika Katiba ile ya kitambo tuliyoiondoa mwaka wa 2010, wakati huo hata Taita Taveta ilikuwa imetajwa pale kwa masuala haya ya ardhi za kijamii. Tulikuwa na wasiwasi sana kuwa sasa hivi vile jina letu limeondoka kwenye Katiba, suala hili litakuwa vipi. Tulivyokuwa Bunge la Kumi, tulivyokwenda Mombasa kuweza kukubaliana kama Wabunge hatukuweza kukubaliana maanake kila mtu alikuwa anamuangalia mwenzake na kumuota kidole akiwa na wasiwasi kuwa, je hawa wanafikiria nini ama wanatupangia njama gani? Hivyo basi, sheria hii ikishakubalika na ninaomba na nitashukuru ya kwamba Bunge la Seneti halitakwenda kubadilisha masuala haya mengi ambayo yamezungumziwa, itawezesha Wakenya kusonga mbele na haswa kutuliza kidonda hiki ambacho kimekuwa kikikera Wakenya wengi. Natoa shukrani kwa Wabunge wote kwa kazi nzuri ambayo wamefanya na haswa wewe kwa kuweza kukaa mpaka saa hizi, saa za usiku ambapo ungekuwa umeenda nyumbani tayari kufanya shughuli zako zingine kwa sababu jamii pia zinangojea. Ninawashukuru wenzangu wote ambao tumekaa hapa mpaka sasa hii. Sheria hii itatuwezesha kama Wakenya kuweza kusonga mbele. Naunga mkono."
}