GET /api/v0.1/hansard/entries/650748/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 650748,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/650748/?format=api",
"text_counter": 42,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, kwa mujibu wa Kifungu 45 (2) (b) cha Kanuni za Seneti, naomba taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Kilimo kuhusu mtambo wa korosho wa Shirika la Kenya Cashew Nuts Limited. Katika taarifa hiyo ningependa Mwenyekiti wa Kamati kueleza:- (1) Je, ni kwanini mtambo wa shirika la Kenya Cashew Nuts Limited uliokuwa kwa mikono ya vyama vya ushirika wa ukulima wa zao la korosho katika Kaunti ya Kilifi ulipewa kampuni ya Millennium Management Limited? (2) Je, ni nani aliyechukuaa asilimia 35 ya hisa walizokuwa nazo wakulima wa korosho wa Kaunti ya Kilifi kwenye shirika la Kenya Cashew Nuts Limited? (3) Je, hisa hizo ambazo ni asilimia 35 ziko wapi na zitarejeshwa lini kwa wale wakulima wa Kilifi? (4) Je, uhamishaji wa hizo hisa za ununuzi wa Shirika la Kenya Cashew Nuts Company Limited ulifanywa kulingana na sheria za Kenya na kama ni hivyo, ni nani aliyeidhinisha kuuzwa au kuhamishwa kwa hisa hizo asilimia 65 zilizomilikiwa na Serikali kwenye Shirika la Kenya Cashew Nuts Limited hadi kwa kampuni ya Kenya Assets Management Limited? (5) Je, Serikali itaweza kurejesha hekari 350 za shamba iliyojengewa lile Shirika la Kenya Cashew Nuts Limited kwa sababu inaonekana wazi kwamba kampuni ya The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}