GET /api/v0.1/hansard/entries/650816/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 650816,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/650816/?format=api",
    "text_counter": 110,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Nawapongeza wenzetu kutoka mashinani kwa kufika hapa. Naamini kwamba watajifunza mengi, kama vile sera za Seneti hii. Ningependa kusisitiza maneno ambayo yamesemwa na wenzangu kuhusu sera za watu kuandamana na kupiga firimbi. Mbiu ya mgambo ikilia kuna jambo. Ukifika kwa kichaka na usikie ndege wengi wakipiga kelele labda kuna nyoka. Ningependa kuwaambia wenzangu walioko upande wa Serikali kwamba mimi nastahili kuitwa mzee kwa sababu ya umri wangu. Kwa hivyo, wanafaa kusikia wosia wangu."
}