GET /api/v0.1/hansard/entries/651308/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 651308,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/651308/?format=api",
"text_counter": 249,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika wa Muda. Pia, mimi natoa rambirambi zangu binafsi na familia yangu, watu wa Kaunti ya Kilifi na vile vile watu wa Shirika la Wakulima nchini Kenya – Agricultural Society of Kenya. Pole kubwa kwa Mzee Kibaki na familia yake kwa kumpoteza mama wa tatu wa taifa katika Jamhuri yetu ya Kenya, Mama Lucy Kibaki. Tunaomba Mwenyezi Mungu ampe Mzee Kibaki na familia yake faraja, ili kukabiliana na msiba huu mkubwa uliompata. Watu wa Kilifi tunasema pole sana kwa Mzee Kibaki. Nilimfahamu Mama Lucy Kibaki nilipokuwa Mwenyekiti was Shirika la Wakulima Nchini. Wakati mwingi alipokuwa na uzito wa kupanda gari la Amiri Jeshi Mkuu wakati Mwenyekiti anapoandamana na Rais na kuzunguka katika maonyesho ya kilimo, ndio wakati nilikuwa nikikaa na yeye tukizungumza huku tukitizama maonyesho ya wakulima. Nakumbuka wakati huo nikiwa Mwenyekiti, hotuba za kitaifa zilikuwa zikitolewa na Mwenyekiti kwa Kiingereza. Mama Lucy wakati mwingi aliniambia: “Ikiwezekana, toa hotuba yako kwa Kiswahili kwa sababu mimi ninapenda vile unaongea Kiswahili.” Nyakati hizo tulikuwa tukicheka sana kwa sababu alikuwa mcheshi zaidi huku akiniuliza: “Mnasemaje neno hili kwa Kiswahili?” Kwa hivyo, tulikuwa watu wa karibu sana kwa ile miaka tatu nilipokuwa Mwenyekiti wa chama hicho. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}