GET /api/v0.1/hansard/entries/654160/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 654160,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654160/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii ya kuchangia Mswada huu. Mswada huu utaokoa nchi yetu kutokana na walaguzi ambao wametuharibia mimea yetu ama mbegu ambazo zilikuwa tegemeo la mwananchi tangu abu na abu. Maradhi ambayo yanakumba nchi hii hivi sasa ni maradhi ambayo wakati wa wazee wetu hayakuwa. Kwa mfano, kuna saratani. Saratani na ugonjwa wa Kifua Kikuu ni maradhi ambayo yalikuwa yakishika milango fulani lakini sasa yamekuwa maradhi ambayo yanashika watu ovyo ovyo. Hii inatokana na yale madawa yanayotumika katika kuchanganya mbegu ambazo zinaletwa na wenzetu ambao wanasema kwamba wameelimika zaidi kushida Waafrika."
}