GET /api/v0.1/hansard/entries/654161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 654161,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654161/?format=api",
    "text_counter": 103,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Mswada huu utalinda mbegu na mimea yetu, na kulinda tamaduni na desturi zetu kama Waafrika wa Kenya. Miti na mimea ilikuwa ni ya dawa, chakula na kivuli. Hivi sasa, ile mimea tunayoletewa kwa kisingizio kwamba ndiyo mimea bora, imeharibu mazingira. Kwa mfano, huko Kwale, katika sehemu ya Marere, wakati sisi tulipokuwa wachanga, Mto Marere ulikuwa haukauki maji. Lakini, wakati ulipopandwa miti iliyoko sasa hivi, ilikuwa chanzo cha ule mto kukauka mpaka leo. Kuna shida kubwa ya maji katika maeneo yetu."
}