GET /api/v0.1/hansard/entries/654164/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 654164,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654164/?format=api",
    "text_counter": 106,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 751,
        "legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
        "slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
    },
    "content": "Kuna masuala ya vyakula. Ni kweli, Serikali yetu, kupitia Bunge, iliweza kuzuia vile vyakula ambavyo vinatokana na mchanganyiko wa madawa. Ni haki vile vyakula vizuiliwe kwa sababu vimeua hadhi ya vyakula vyetu vya kitamaduni. Ninakumbuka nyanya yangu alifariki akiwa na umri wa miaka 126. Alikuwa anaona na kula nyama na mahindi kwa sababu alikuwa na meno yote. Mtoto wa miaka 35 leo, hata meno yameisha mdomoni kwa sababu ya vyakula ambavyo tunakula. Vyakula vyote viko ndani ya mkebe na vina madawa ambayo hatuyaelewi yametokana na nini. Hii ni hatari kubwa kwa afya zetu."
}