GET /api/v0.1/hansard/entries/654185/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 654185,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654185/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii. Kabla niongee kuhusu Mswada ulio mbele yetu, ninataka kusalimia Waheshimiwa wenzangu. Nimeambiwa niwasalimie na watu wa eneo la Uwakilishi Bunge la Ruiru. Yafaa tuungane na akina mama katika mambo yaliyo mbele yetu. Ninaunga mkono nikisema kwamba mara nyingi tunafanya mambo na kukosea kwa kukosa kuelewa. Kama vile wenzangu wamechangia mbeleni, ni vizuri tuangalie mimea na hata mbegu ambazo ziko katika nchi yetu ya Kenya. Kile kitu tulicho nacho na labda tunadharau ni kwamba tunaona vifaa vya ugenini vikiwa muhimu kuliko vile tunavyo hapa. Ninatazama runinga sana. Nilikuwa ninaona mzee mmoja upande wa Maasai. Wakati pombe iliisha, alianza kupika supu na kuweka mizizi ya miti ambayo alisema ilikuwa na dawa ndani yake. Kusema kweli, niliona laini kubwa sana. Kila mtu alikuwa anataka kuonja hiyo supu. Wale walikuwa wanakunywa walikuwa wanasema miili yao imekuwa sawa. Wanaume walikuwa wanasema hata “ transformer ” ziko sawa. Habari hizo zilikuwa kwa runinga. Inamaanisha kwamba kuna mambo mengine tunadharau na kuchukulia tu kama mambo ya kijiji. Jambo lingine ambayo niliona kwa runinga ni kwamba kuna mzee----"
}