GET /api/v0.1/hansard/entries/654192/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 654192,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654192/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Nilinde Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninafikiri hilo jambo limewafurahisha sana. Wengi wamesoma na wanajua kuhusu mimea ambayo tuko nayo. Kile kitu tunakosa ni watu wa kueleza wananchi wa kawaida kuhusu yale maoni ama masomo ambayo wamesoma. Saa zingine tunaidharau hiyo mimea kwa sababu tunaona kama mimea ya kiasili imeisha. Ningeomba kila mtu atilie maanani hiyo mimea na tuilinde ndiposa tuweze kuendelea. Wakati mwingi hata ukiwa na ugonjwa unaambiwa ukichemsha majani haya na unywe maji yake labda utakuwa sawa. Wengine, hasa mimi, saa zingine tunaambiwa kwamba tumbo zetu ni kubwa na kwa hivyo tunywe maji ya majani fulani, na hayo majani yametoka ugenini. Labda yalitoka kwetu, yakapelekwa ugenini na kurudi. Kwa hivyo, ni vizuri hata sisi tuheshimu mimea ambayo iko hapa nchini ndiposa tukifanya kitu, hata sisi tunajivunia kuwa na mimea ambayo inatusaidia. Tunaweza kuhifadhi hata wakati kuna njaa na hatutakimbia hapa na pale tukiomba mbegu za kupanda na chakula cha kula. Ni vyema tuwe nazo ili tuweze kuzilinda na kuzihifadhi. Mheshimiwa, ninaomba unione nikitoka nje."
}