GET /api/v0.1/hansard/entries/654238/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 654238,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654238/?format=api",
    "text_counter": 180,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Changorok",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1149,
        "legal_name": "Regina Nyeris Changorok",
        "slug": "regina-nyeris-changorok"
    },
    "content": "zingine ambazo zinamea kwa haraka. Lakini, hata hivyo, zinaweza kuharibu na kuadhiri afya ya wananchi. Kuna mimea ambayo ni chakula and kuna mimea ambayo ni dawa. Hapo zamani, ugonjwa wa homa ya matumbo ulikuwa ukitibiwa na pombe aina ya busaa. Watu walitumia busaa hata kwa mtoto akiwa na ugonjwa huo. Walikuwa wanampatia huo mvinyo na anapona. Pia, wakifinya machicha ya pombe hiyo, walipaka kwenye sehemu yoyote ya mwili ambayo iko na shida na watu walipona. Ni kitu rahisi ambacho kinachukua muda mfupi na hakidhuru mwili. Kuhusu sayansi, kuna ulegevu na kutojali ama kutofikiria vizuri. Wanasayansi wetu wangechukua muda kufikiria na kuchukua mbegu hizo ili kuchanganya na zingine. Labda tungepata mbegu nzuri zaidi ambazo zingemea kwenye sehemu mbali mbali za nchi. Kuna mambo fulani ya Mswada huu ambayo siungi mkono. Nitaungana na Mhe. Odhiambo-Mabona kuleta mabadiliko mazuri. Kwa hivyo, mbegu zetu za kiasili ni lazima tuziangazie zaidi. Lazima tuangalie na kuona ni mimea gani inaweza kumea kwa haraka kwa sababu ya hali mbaya ya hewa na mvua dogo. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, naunga mkono Mswada huu."
}