GET /api/v0.1/hansard/entries/654254/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 654254,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654254/?format=api",
"text_counter": 196,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Rai",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": "Mhe. Naibu Spika wa Muda, naomba kuunga mkono Mswada huu na kuiombea kuwa sheria. Sisi ambao tumetoka eneo kame na mahali ambapo maji ni shida, hatukuwahi kuiona kiliniki. Tuliishi kutumia madawa ya kienyeji. Hivi sasa, wanatekinolojia wanaona kwamba ni vyema kuwa na kituo kama hicho ambacho kinaweza kuleta utafiti na kuboresha mambo kama haya ili yaweze kunawiri. Ningependa kulipongeza suala hilo kwa sababu enzi zile za nyuma, tulikuwa tukitegemea mavi ya ndovu kutibu homa. Yalikuwa yakiwekwa kwenye makaa na tungewekwa karibu na ule moshi. Tulinawiri na tumefika pahali ambapo tumefika. Tumeharibiwa masuala mengi na mzungu aliyetutawala pia kiakili. Imefika mahali ambapo tunaona kuwa kila kitu kitokacho ardhi ya Mwafrika hakiwezi kuwa cha msaada. Kituo kama hicho kitakapoanzishwa na kutambua mbegu na mimea inayoweza kuwa ya faida katika nchi hii, kitasaidia Wakenya au Waafrika kuliko sisi kutegemea kwamba mpaka twende Uchina tupewe nyasi na tukubali kuwa ni dawa na labda nyasi zile zinapatikana nchini. Ukweli ni kwamba tunavidharau vitu vyetu lakini tukipata mwelekeo wa kuviboresha, ni suala ambalo tunaweza kujivunia ili tukatambue tunakotoka na tunakokwenda. Nina imani kuwa jinsi Mswada huu unavyoungwa mkono, hata ijapo mapendekezo madogo madogo yatakayofanyiwa ukarabati kwenye Kamati, huenda ukawa nguzo ya kutegemea na kuhakikisha kwamba nchi hii inarudi katika barabara ya kujitambua. Ni rahisi kwa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}