GET /api/v0.1/hansard/entries/654255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 654255,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654255/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Rai",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": "binadamu kusema kwamba amejitoa katika minyororo ya wakoloni, lakini ukoloni unaendelea kumsumbua akilini. Katika Vitabu vya Mwenyezi Mungu, Biblia na Quran, tuliwahi kuambiwa kuwa miti mingi ni dawa. Zama zile, tulipokumbana na nyoka, hatukupelekwa hospitalini kwa sababu nyoka angesemewa na kusikia na sumu ingesimama mahali ilipokuwa. Uwezo huo ulikuweko na labda utafiti wa kuboresha hali hiyo unakosekana. Naunga mkono kwamba kituo hicho kitakapoanzishwa, kipewe pesa kwa sababu kuna vitu viwili. Tupitishe na kiwe kituo cha kufanya utafiti lakini tukikosa kukipa pesa, itakuwa tumejenga nyumba ambayo haina wanadamu ndani. Naunga mkono na kutia sauti kwa wale wengi ambao walikuwa tayari wameunga mkono Mswada huu."
}