GET /api/v0.1/hansard/entries/654329/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 654329,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/654329/?format=api",
"text_counter": 58,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 379,
"legal_name": "Maison Leshoomo",
"slug": "maison-leshoomo"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Spika, kwa kunipatia nafasi hii pia niseme pole kwa familia ya Rais Mstaafu, Mwai Kibaki, na watoto wake. Kila Mkenya anajua kuwa niko hapa Bunge kwa sababu yake. Siku yake aliyowekewa na Mwenyezi Mungu imefika na tunasema pole. Pia, natoa pole kwa niaba ya Wasamburu wote. Alipofika Samburu, aliangalia na akajua kuwa kuna kiongozi na akanichagua kati ya Wasamburu. Hakuna mwanaume Msamburu aliyejua kuwa kuna kiongozi mwanamke Msamburu. Kwa hivyo, ile baraka alipea Wasamburu na kile ameonyesha Wasamburu ni kwamba mwanamke anaweza kuwa kiongozi. Hatutamsahau hata kama Mwenyezi Mungu amemchukua. Ni mama tutakayemkumbuka kwa yale ametufanyia. Nasema pole kwa familia. Tutakuwa pamoja kwa yote watakayofanya. Ahsante."
}