GET /api/v0.1/hansard/entries/656184/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 656184,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/656184/?format=api",
"text_counter": 181,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kunipa nafasi kutoa mawazo yangu kuhusu Mswada huu wa kurekebisha Katiba kuhusu wasio na uwezo katika jamii yetu. Ni kudra ya Mungu kuzaliwa ukiwa na uwezo au kuzaliwa kilema. Mtu yeyote anaweza kuzaliwa akiwa mzima na kujipata amelemaa kutokana na ugonjwa, ajali au maumbile yake. Kwa hivyo, hata wale ambao wana uwezo wasije wakaringa kwa sababu wao pia wanaweza kujipata katika kundi la walemavu. Ni kudra ya Mungu mtu kuishi na kumaliza miaka yake bila kulemaa. Mungu akikubariki uishi hadi uzee wako, huenda ukapofuka, ukawa kiziwi au upate shida ya miguu kwa sababu ya uzee. Hapo utakuwa umelemaa.Kwa hivyo, lazima tujue kwamba mtu yeyote anaweza kujipata katika hali hiyo wakati wowote. Kipengele 54(1) katika Katiba yetu ya Kenya kinatoa haki kwa wale wasio na uwezo kamili kwa njia yoyote ile. Wao wana haki ya kujumuika na wengine, kutunzwa na kuangaliwa kwa heshima. Mazingira, lishe na makazi yao yanafaa kuazingatiwa. Wanafaa kuishi kwa heshima. Mswada huu unapendekeza vigezo vya kamati au halmashauri ambayo itasimamiwa na wasio na uwezo. Kamati hiyo itajumuishwa kikamilifu na serikali za kaunti. Lengo ni kuhakikisha kuwa nafasi mwafaka ya wasio na uwezo kuwakilishwa kikamilifu imepatikana. Sheria hii itahakikisha kwamba kuna uwakilishaji wa wasio na uwezo kutoka mashinani hadi Serikali ya kitaifa. Hivyo basi, Mswada huu unalenga kuongeza Sehemu 2(a) ambayo itatoa sheria na sera za kuwatunza wasio na uwezo, kuchunguza na kutangaza masilahi yao. Sehemu 2(b) inahitaji kuwe na uchunguzi kamili kujua kwa nini na kwa sababu gani watu hulemaa. Tukijua sababu, basi tutajua kinga.Hata hivyo, kuna sababu kadhaa zinazosababisha mtu kulemaa ambazo tunaelewa.Zingine ninaweza kuepukika. Hizi ni kama vile kutokuwa na zahanati za kutosha kwa kina mama kujifungua salama na kuzaa watoto wazima. Utapata kuwa wakati mwingine, mama hawezi kufanyiwa upasuaji au hakuna dakitari aliye na uwezo wa kujua kwamba mtoto ana shida. Kwa hivyo, utapata kuwa mtoto anazaliwa mbumbumbu, hali ambayo ingeepukwa. Kuna hali zingine za kulemaza kama vile poliomyelitis . Chanjo kwa watoto wasiozidi miaka mitano imesisitizwa sana nchini. Ni wito wangu kwamba kila jamii iwapeleke watoto kupata chanjo.Najua kwamba kuna sera za dini zingine nchini ambazo zinawanyima watoto haki hii. Bw. Spika wa Muda, sababu nyingine ni ajali. Kwanza, nipe nafasi nitoe rambirambi zangu kwa wale waliopoteza maisha yao huko Huruma kwa sababu ya uzembe wa mafundi, wahandisi na Serikali. Serikali iliruhusu ujenzi wa nyumba hafifu na kisha kuruhusu binadamu aishi ndani ya nyumba hiyo. Uzembe na ufidhuli ni mambo ambayo hayakubaliki kabisa. Sheria hii itatupa uwezo wa kuchukua hatua ya kukabiliana na mambo kama hayo ambayo yanasababisha watu kulemaa. Sheria inasema kwamba walemavu wanapaswa The electronic version of theSenate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}