GET /api/v0.1/hansard/entries/656186/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 656186,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/656186/?format=api",
    "text_counter": 183,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kupewa vifaa na washughulikiwe na watu ambao wamesoma na kukomaa. Pia, wapewe vifaa vya kufanya mazoezi ili warudi katika hali nafuu. Hata kama sio hali ya uzima kabisa, lakini angalau iwe hali ya kujitegemea. Sheria hiyo inatoa nafasi ya watu waliolemaa kupata nafasi ya kujumuika na wengine shuleni na hata kazini ndani na nje ya Serikali. Watu hawa wanatakiwa kuwa na uwezo wa kupata elimu, haki zingine na kadhalika. Kila mtoto apewe nafasi hiyo. Kwa hivyo, mambo haya lazima yatekelezwe kwa mujibu wa sheria ya serikali kuu na ya kaunti. Kwa kila kaunti, inatakikana kamati iundwe ili kutoa ushauri kwa mambo yanoyowahusu watu waliokosa uwezo mmoja au mwingine. Mimi sitaenda kwa undani zaidi na kusema hizi kamati ziwe na akina nani. Ninapendekeza tu kwamba katika kamati hizo, lazima kuwemo watu wasiopungua wanne kutoka hii jamii ya walemavu. Baraka huja kwa njia nyingi. Tunaweza kupigwa sisi hapa Bungeni tusipopendekeza au kuratibisha Miswada kama hii, ili itumike kuwakuza walemavu kwa njia ya haki na wawe na furaha. Nina budi kwa dhati kuunga mkono marekebisho ambayo yamependekezwa kwa Mswada huu."
}