GET /api/v0.1/hansard/entries/656201/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 656201,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/656201/?format=api",
"text_counter": 198,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, asante kwa kuniita kwa majina hayo yote ambayo nayakubali kabisa. Asante kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia Mswada huu unaohusu walemavu. Kama tunavyojua, kila kinachozaliwa hakikosi kasoro.Wengine wetu tulibahatika kazaliwa bila ulemavu.Kuna watu walemavu katika familia nyingi katika taifa la Kenya.Ni lazima tukubali maumbile ya mwenyezi Mungu. Kuna watu wanaozaliwa na ulemavu and wale wanaopata ulemavu kutokana na ajali mbalimbali. Tuko na ndugu zetu kama vile Sen. Leshore, ambaye alizaliwa bila ulemavu lakini alipata ajali iliyomuweka katika hali ya ulemavu. Vile vile, watu wengine hupata ulemavu kutokana na magonjwa mbalimbali. Bw. Spika wa Muda, Serikali yetu imelegeza kamba kidogo kwa kuwasaidia walemavu. Pia, kuna vyombo vya habari ambavyo haviwasaidii walemavu. Kuna baadhi ya stesheni za televisheni ambazo hazina waelekezi wa watu walio na ulemavu wanapopeperusha vipindi vyao. Vile vile ni aibu kuona ya kwamba watu walemavu hawawezi kuingia kwenye majengo fulani nchini. Hata tulipokuwa Watamu hivi majuzi ilibidi tumbebe mmoja wetu, Sen. Omondi, ili aweze kuingia ndani ya chumba cha mikutano. Kuna hoteli kubwa kama vile Intercontinental Hotel ambayo ina upungufu wa vifaa vya kuwasaidia walemavu. Vile vile, Serikali zetu za mashinani zinapojenga shule za chekechea hazizingatii watoto ambao wako na ulemavu. Tunasisitiza ya kwamba shule hizo na taasisi mbali mbali ni lazima ziwe na vifaa maalum kama njia za kutumiwa na watu walemavu. Inasikitisha kwamba kuna baadhi ya makanisa na misikiti ambako watu walemavu hawawezi kuingia bila kubebwa. Mambo kama haya yanaleta utata na ni The electronic version of theSenate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}