GET /api/v0.1/hansard/entries/656203/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 656203,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/656203/?format=api",
    "text_counter": 200,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "lazima tuweke sheria kama hizi. Ninauhakika kwamba sheria hizi zitawasaidia walemavu. Bw. Spika wa Muda, tunawapenda wanawake wetu na tungependa kila mmoja wao apate mtoto. Kuna wanawake wanaojiweza na hivyo wanaweza kupanda kitanda wakati wa kujifungua. Hivyo hivyo, kuna wanawake walemavu walio wajawazito. Ikifika wakati wa kujifungua, hospitali nyingi hazina vitanda vya wanawake walemavu. Inawabidi kulala sakafuni, ukarabati ubuniwe na wakunga ili waweze kujifungua. Hospitali zinafaa kutia maanani urefu wa vitanda ili wanawake walemavu waweze kuvipanda na kujifungua kwa njia rahisi. Hivi majuzi, sehemu nyingi za nchi yetu zimepata hasara kutokana na mvua haswa mtaa wa Huruma. Kutokana na mkasa huo, huenda waathiriwa wengine wakawa walemavu. Je ni hatua gani Serikali inachukua kuhakikisha kwamba hatua inachukuliwa dhidi ya watu wanaokarabati nyumba za hali duni hivyo kuongeza idadi ya walemavu? Ni sheria gani itabuniwa ili kutoa adhabu kali kwa watu wanaotengeneza nyumba bila kukarabatia vizuri na kuweka nafasi za watu walio na ulemavu kuingia katika nyumba hizo. Ni lazima tuweke sheria kali dhidi ya ukarabati duni kama lile jengo lililoporomoka hivi majuzi."
}