GET /api/v0.1/hansard/entries/657804/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 657804,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/657804/?format=api",
"text_counter": 733,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2308,
"legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
"slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipatia nafasi hii ili niunge mkono Hoja iliyoko mbele yetu siku ya leo. Ni lazima Serikali itafakari kwa sababu mara nyingi huwa na zogo kwa sababu ya hawa watu wa IEBC. Ingawa mmoja wetu hivi sasa amezungumza na kuuliza watu wa CORD wako wapi, nataka kumwambia ya kwamba mambo haya si ya CORD. CORD inasimamia haya mambo na yoyote anayezungumza ana simamia mambo haya kwa sababu ya kuleta amani nchini. Kwa hivyo, awe mtu wa CORD ama Jubilee mimi naona kwamba iko haja jambo hili liangaliwe kwa makini na watu wote ili kuondoa ghasia na matatizo ambayo mara kwa mara yanazushwa kwa sababu ya IEBC. Kwa hivyo IEBC lazima iangaliwe kirefu na kupigwa msasa na wachukie watu waadhilifu ambao wanajua wanafanya nini na ambao imani yao ni kuhakikisha kwamba Kenya imekuwa na amani. Nikirudi katika upande wa elimu, fikira zangu naona ya kwamba, ni vizuri zaidi turudi kwa zile nyakati za nyuma na twende kufanya mitihani na mtu akipita Kiswahili ama Kingereza aende moja kwa moja kwa uchaguzi. Kwa sababu kuna watu wengi wana makaratasi na mwisho unasikia hayo makaratasi ni ya wizi, si ya haki. Kwa hivyo mtu akiwa bayana pale anafanya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}