GET /api/v0.1/hansard/entries/657812/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 657812,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/657812/?format=api",
    "text_counter": 741,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Bunge hili huwa na matatizo wakati Mwanyoha anazugumza. Watu hutoa maneno ili wakati wangu uishe. Mhe. Naibu Spika wa Muda, nashukuru kwa kunitetea; uendelee namna hiyo. Nataka sasa niongee kuhusu nambari ya wale ambao wanahitajika kupiga kura katika kituo. Mara kwa mara kuna watu wengi sana, mpaka watu wengine huja saa kumi na mbili za asubuhi. Lakini ikifika saa kumi na mbili za jioni wanaambia wakati umeisha na wanaachwa nje. Naomba kuwe na marekebisho ili badala ya kuwa na watu 1,000 wawe 500 kwa kila kituo. Vituo viweze kuongezwa ili kuwe na muda mrefu na kila mtu aweze kupiga kura.Kwa hivyo naomba Serikali ihakikishe kwamba itaongeza vituo na nambari ya kila kituo iwe ndogo. Nikirudi kwa uteuzi wa wale Wabunge ama madiwani ambao wanataka kuchaguliwa au kuteuliwa, hii iwe baada ya uchaguzi ili tuweze kuangalia ni nani alikuwa anafanya kazi nzuri wakati wa kampeini na nani alikuwa goigoi. Kwa sababu wengine huketi bure na mwisho huchaguliwa bila kuangalia na wengine wanaenda kiasi cha kuchagua wapenzi wao. Kwa hivyo mimi naomba hii ifanywe sawa."
}