GET /api/v0.1/hansard/entries/659448/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 659448,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/659448/?format=api",
    "text_counter": 360,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Gichigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1909,
        "legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
        "slug": "samuel-kamunye-gichigi"
    },
    "content": "Naibu Mhe. Spika wa Muda, naomba unilinde kutokana na Mhe. Duale, ambaye anapiga kelele sana upande huu. Kuhusu Tume ya Uchaguzi, ningependa kusema kwamba siku ambayo watu fulani watakuja kwenye lango la Bunge na kusema wanataka kutufurusha kutoka Bungeni kwa sababu tumeshindwa kufanya kazi yetu, ndiyo tutaelewa ni nini Wapinzani wetu wanafanya. Pia, wakati watoto wao wataenda kwenye shule zao na kusema kwamba wanataka kuwafurusha walimu wote kwasababu shule hizo hazijafanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa, ndiyo tutajua ni nini tunaonyeshwa na hao maadui wa nchi hii."
}