GET /api/v0.1/hansard/entries/659598/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 659598,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/659598/?format=api",
"text_counter": 135,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Gichigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1909,
"legal_name": "Samuel Kamunye Gichigi",
"slug": "samuel-kamunye-gichigi"
},
"content": "Nakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nina furaha tumeweza kuupitisha Mswada huu ulioletwa Bungeni leo kupitia kikao hiki spesheli. Tuna wanariadha au wakimbiaji na wanamichezo wengi kule Kipipiri. Walikuwa wameanza kupata wasiwasi kuwa huenda nchi yetu isipewe nafasi ya kwenda kwa nashindano ya Olimpiki. Tukiangalia yale yamefanyika kuhusiana na hii sheria, ni kweli kuwa Kenya inaonewa na mataifa yale makubwa yasiyoamini kuwa nchi ndogo kiuchumi kama Kenya inaweza kuwa ikiongoza katika mashindano. Katika mashindanao ya dunia ya riadha yaliyopita, Kenya ilikuwa namba moja. Naona kama shida za Kenya zilianzia hapo. Kwa hivyo, tunawaomba World Anti-Doping Agency (WADA) waache kuangalia Kenya kwa sababu ya ushindani wake. Tunastahili kutwikwa zawadi na medali na sio mambo ya kukimbizwa-kimbizwa. Mwishowe, inajulikana kuwa Kenya huchukua zaidi ya asilimia kubwa ya medali katika mbio za nyika."
}