GET /api/v0.1/hansard/entries/661447/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 661447,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/661447/?format=api",
    "text_counter": 336,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "Hivyo pia, itakuwa ni nafasi kwa nchi kujiongezea mapato yake. Kufikia hivi sasa, Bandari ya Mombasa inachangia hela nyingi kwa uchumi wa taifa. Kwa hivyo, kupinga Hoja hii ni hatua ya kurudisha nyuma maendeleo. Tukisema kwamba hata vile vilivyoko bado havijatumika kikamilifu ni sawa na kusema ya kwamba kwa sababu mwaka ujao tutajenga shule zingine hakuna haja tupanue zile shule zilizoko. Hayo ni mawazo duni na siyatazamii kuzungumziwa na waheshimiwa katika Bunge hili. Kwa hayo machache, naunga mkono Hoja hii."
}