GET /api/v0.1/hansard/entries/661511/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 661511,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/661511/?format=api",
"text_counter": 400,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2100,
"legal_name": "Shariff Athman Ali",
"slug": "shariff-athman-ali"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Kwa kweli, Hoja hii ni ya kushangaza. Kuzungumza kuhusu Bunge hili kupitisha mkopo wa Kshs27.3 bilioni ni jambo la kushangaza. Huu mradi ambao unafanyika Mombasa ni mradi ambao tukiwa watu wa Pwani na Wakenya, tungependa uwe kwa sababu ya kuinua uchumi wa nchi hii na uchumi wa Pwani. La kushangaza ni kwamba jambo hili limeletwa Bungeni ilhali mradi huu unaendelea. Ninashindwa pesa hizi zilikuwa zimepangiwa kulipwa namna gani ilhali huu ni mradi ambao tayari umeanza. Isitoshe, linalonishangaza ni kwamba mbali na kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuinua uchumi wetu, ni vipi tutaweza kusaidia sehemu zingine kuinua uchumi wake kuliko kusema tunapeleka pesa mahali Fulani? Kuna miradi ambayo imekwama kama vile mradi wa LAPSSET. Ukizungumza kuhusu LAPSSET, unaambiwa kuwa tatizo ni pesa. Huu ni mradi ambao kwa imani yangu Serikali ikiekeza pesa zake unaweza kusaidia pakubwa uchumi wa nchi hii. Lakini lanishangaza pakubwa leo kuona kwamba Bunge hili lahitajika kupitisha Hoja hii ili pesa zilipwe hili shirika la Kijapan ili kutekeleza mradi huu."
}