GET /api/v0.1/hansard/entries/661512/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 661512,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/661512/?format=api",
    "text_counter": 401,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. S.A. Ali",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2100,
        "legal_name": "Shariff Athman Ali",
        "slug": "shariff-athman-ali"
    },
    "content": "Kwa kweli, hatuwezi kukataa maendeleo yasifanyike, na tukiwa kama viongonzi tuna kila haki kuhakikisha kwamba tumesaidia nchi hii katika swala nzima la uchumi wetu. Lakini, mambo mengine kama haya yanahitaji maswala mengi kutoka kwetu sisi viongozi. Kwa mfano, tunasema kwamba tutachukua takribani miaka 34 kulipa deni hili na ilhali tuna uhakika KPA ni shirika moja katika nchi hii linaloingiza pesa nyingi sana. La ajabu ni kwamba leo Serikali inajiongezea madeni kama haya, na nina imani kwamba mzigo huu utakuwa wa wananchi. Hili linatendeka ilhali ushuru unaotozwa mizigo katika bandari ni wa juu. Baadaye wanaoleta bidhaa ama kufanya biashara katika nchi hii wanalipa ushuru ule na kuongeza bei za bidhaa ambazo wameleta."
}