GET /api/v0.1/hansard/entries/661565/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 661565,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/661565/?format=api",
"text_counter": 454,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 631,
"legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
"slug": "rachel-ameso-amolo"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninasimama kuunga mkono Hoja hii kwa sababu tumeona vile NGCDF ilivyosaidia Wakenya wengi, hasa maendeleo katika maeneo Bunge yetu hapa Kenya. Mahali popote unatembea, lazima utaona jengo lililo na alama ya NGCDF. Hili ni jambo nzuri sana kwa sababu linatuonyesha Wabunge wetu wanatumia pesa hizo kwa njia inayofaa. Lingekuwa jambo zuri pia ikiwa kaunti zingeiga mfano wa NGCDF ili magavana wetu wasiwe wanaambiwa saa zote wazitumie zile senti bali wawe na kamati ambayo itatoa mipango ya vile zile pesa zinaweza kutumika. Ni jambo lakushangaza unapopata Wakenya wengine wanaenda kortini kupinga NGCDF na zile fedha ambazo zinatengewa wawakilishi wa akina mama pia. Ninashangaa ni Mkenya wa aina gani ambaye anaweza kujitokeza kwenda kupeleka NGCDF kortini na kusema kuwa Wabunge hawafai katakata kuwa na zile senti za NGCDF. Wakenya wakitembea mahali popote nchini wataona alama za NGCDF na watajua hizo pesa zimetumika vizuri. Vile vile, ningependa ninawajulishe Wakenya kuwa si Mbunge anayehifadhi pesa za NGCDF bali ni kamati ambayo imeteuliwa. Kwa mfano, leo hapa Bungeni tumeona maeneo bunge ambayo tayari yamewasilisha kamati zao za NGCDF. Maeneo Bunge ya Nyakach, Lafey na Isiolo sasa wanakamati wao wanajulikana. Ikiwa pesa za NGCDF hazitatumika katika njia inayofaa basi itakuwa ni hao wanakamati wa maeneo bunge hayo ambao wamezitumia kwa njia isiyofaa, na hao ndio watakaokuwa na jukumu la kueleza vile hizo pesa zimetumika. Ukitembea katika shule mbalimbali, utapata watoto ambao wamesaidiwa na hizo pesa za NGCDF.Wengi wao wamesoma kwa mujibu wa zile pesa za NGCDF. Kwa hivyo, ni vizuri NGCDF iendelee kusaidia katika elimu na usalama. Pesa hizi ndizo zinazowasaidia watoto wetu sana kumaliza masomo yao shuleni na kujiunga na vyuo vikuu. Tunasema hivi, NGCDF na zile pesa za wawakilishi wa akina mama ziweze kuendelea ili sote pamoja kama viongozi katika nchi yetu ya Kenya tusaidie wananchi wetu kuweza kuendelea na mijengo ya shule ili iwe ya kisasa. Tumeona mabadiliko makubwa sana. Ukitembea katika eneo Bunge la Kibra utaona shule zimeinuka kabisa na zimeweza kuchukua hatua nyingine kwa sababu ya NGCDF. Vile nimesikia na kushuhudia Mbunge wa eneo Bunge la Budalang’i akisema NGCDF ndio imewezesha wao kuwa na chuo kikuu katika Budalangi. Ninataka kumuunga mkono sana na Wabunge wengine waweze kuangalia hizo pesa na wafungue vyuo vingine ambavyo vitaleta faida katika nchi yetu ya Kenya. Kwa hivyo, ninasimama kuunga mkono Hoja hii. Asante sana."
}