GET /api/v0.1/hansard/entries/661988/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 661988,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/661988/?format=api",
"text_counter": 19,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Mheshimiwa Spika, ninasimama kuunga mkono Ombi hili kwani hata mimi sielewi ni kwa sababu gani Waziri alitoa uamuzi kuwa suala la maombi katika shule nchini lipigwe marufuku, hasa katika muhula wa tatu. Sioni uhusiano wowote kati ya sala na udanganyifu wakati wa mtihani. Ndugu yangu, Mhe. Kamama, ninaomba nikujulishe kuwa si vijana ama wanafunzi wanaokaa katika mabweni tu ambao wanaweza kupatikana na hatia kama hiyo. Je, itakuwa namna gani kwa wale ambao wanakuja shuleni asubuhi na kwenda nyumbani jioni ambao hawakai katika mabweni? Ikiwa ni suala la udanganyifu, wao pia wanaweza kupata hayo makaratasi njiani. Kwa hivyo, hiyo si sababu ya kumfanya Waziri kutoa uamuzi bila kuwahusisha wahusika wote. Shida kuu ni kuwa tunatafuta njia ya kusitisha au kuondoa udanganyifu katika masuala ya mitihani kwa kutafuta sababu zingine ambazo hazihusiki na mitihani. Tunamwomba Waziri atafute sababu na njia mwafaka ya kuondoa udanganyifu katika mtihani wetu. Ninakubali kuwa Ombi hili ni la muhimu kwa sababu kuna udanganyifu katika masuala ya mitihani, lakini mbinu ambayo imetumiwa na Waziri ya kusitisha maombi haifai. Kama mnavyofahamu, sala na maombi wakati wa mtihani inatia wanafunzi mori na kuwafanya wamtegemee Mungu katika mitihani yao. Sina habari kama Waziri anajua maombi ni nini wala sijui kama anajihusisha na maombi. Ninaunga mkono Ombi hili na ninamuunga mkono Mhe. Chris kwa kulileta Bungeni."
}