GET /api/v0.1/hansard/entries/661997/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 661997,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/661997/?format=api",
    "text_counter": 28,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": "Jambo hili ni la muhimu katika elimu yetu hapa nchini Kenya. Lakini ningependa kumsihi yule ambaye ameleta Ombi hili hapa Bungeni, Dkt. Chris Wamalwa kuwa ingekuwa vizuri tuhakikishe kuwa hili jambo lililetwe kwa Kamati ya Bunge inayohusika na mambo ya elimu ili tumwite Waziri wa Elimu aje atuelezee ni sababu gani iliyomfanya aamue hivyo. Jambo la mwisho ni kuhusu vile ambavyo Mhe. Dadangu alisema hapa kuwa Waziri Matiang’i ni mzee wa Kanisa la SDA. Ni mzee ambaye anaheshimika na ni Waziri wakati huu. Si vyema kusema kuwa yeye hajui kumwomba ama kuswali kwa Mwenyezi Mungu. Ingekuwa vizuri tumpe nafasi wakati Kamati itakavyoketi, atueleze ni nini kilichomfanya akaamua hivyo."
}