GET /api/v0.1/hansard/entries/662024/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 662024,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/662024/?format=api",
    "text_counter": 55,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Murungi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2802,
        "legal_name": "Kathuri Murungi",
        "slug": "kathuri-murungi"
    },
    "content": "Asante sana kwa fursa hii ya kuchangia hili Ombi la Mbunge mwenzetu. Mhe. Spika, yangu ni machache. Inapaswa hali ya mashamba katika taifa letu iangaliwe upya kabisa. Hii ni kwa sababu tumepata maombi mengi kuhusu mashamba. Kamati yetu ya Ardhi ya Bunge hili letu la Kitaifa inapaswa iangalie mambo ya mashamba kabisa. Zaidi iwe ni kuhusu mashamba yanayohusu wananchi. Ninaunga mkono. Katika eneo la Meru, ninakotoka, kuna shamba kubwa linalotumiwa na Wanajeshi wa Uingereza. Tukiwa viongozi wa eneo hilo, tunaomba wasiruhusiwe tena kuingia kwa hili shamba kwa sababu tungependa tuelewane. Tunataka mmea wetu wa miraa uingie huko Uingereza na tutawapatia hiyo ardhi wafanyie mazoezi yao ya kijeshi. Pia, ninaomba Wabunge watuunge mkono wakati hilo swala litafika kwa hili Bunge ndio tuwe na haya mazungumzo na tuelewane."
}