GET /api/v0.1/hansard/entries/662388/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 662388,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/662388/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ababu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 108,
        "legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
        "slug": "ababu-namwamba"
    },
    "content": "kuorodheshwa ni suala ambalo linapatikana katika kila nyanja. Hata sisi kama Wabunge, tunajua kwamba ukitazama ule utaratibu na utamaduni kwenye Jumuiya ya Madola, utapata ya kwamba hata Wabunge kama sisi huorodheshwa kwenye viwango mbalimbali na kuna utaratibu wa utamaduni huo. Kwa mfano, ikiwa ni lazima utoe nafasi katika mjadala kati ya Mbunge wa kawaida au Mbunge ambaye anashikilia wadhifa fulani katika uongozi wa Bunge hili, utatoa nafasi ya kwanza kwa yule Mbunge anayeshikilia wadhifa fulani ama kwa yule Mbunge ambaye amekuwa hapa kwa muda fulani. Huo ni utaratibu ambao umekubalika katika utamaduni wa Bunge za Jumuiya ya Madola. Utaratibu huu wa kuorodhesha uko hata mbinguni. Kule mbinguni, hata malaika wameorodheshwa. Kuna malaika mkuu ambaye ukifika kule mbinguni, atakufungulia mlango. Hilo ni suala ambalo sisi Wakristo tunalijua sana. Utaratibu huu wa kuorodheshwa tumekuwa nao kwa muda mrefu hapa nchini. Mwenyekiti wangu wa Kamati ya Bajeti anajua suala hili la orodha kule mbinguni. Hili si suala geni katika taifa hili. Tumekuwa na utaratibu huu wa kuorodhesha shule na wanafunzi katika mitihani ya kitaifa, lakini suala hili lilikumbwa na matatizo kwa sababu ya udanganyifu katika mitihani na mashindano yasiyostahili. Shule nyingi ziliiga mtindo ambao mashindano yalifikia kiwango ambacho kilikuwa kufa na kupona. Shule kadhaa zilianza kutumia mbinu potovu ambazo zilipelekea aliyekuwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Tekinolojia, Jacob Kaimenyi, kufutilia mbali utaratibu huu wa kuorodhesha shule na wanafunzi. Lakini mimi ningependa kumkosoa Kaimenyi kwa sababu matatizo hayakuwa katika kuorodhesha. Matatizo yalikuwa katika usimamizi wa mitihani, jinsi Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia inavyosimamia secta hii ya Elimu na jinsi tunavyosambaza rasilmali katika shule mbalimbali katika sehemu tofauti za taifa. Haya ni masuala ambayo Serikali, kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekinolojia, inastahili kuyashuhulikia. Lazima tuwe na usimamizi bora wa mitihani. Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC) lazima lifanyiwe mabadiliko makubwa ili kuhakikisha kwamba linasimamia mitihani kwa njia inayostahili. Sasa tumeingia kwenye mfumo wa ugatuzi. Nimewasikia wenzangu wakichangia Mswada huu. Wameleta tetesi kwamba itakuwa vigumu kuorodhesha shule ilhali kuna hali tofauti katika sehemu mbalimbali za taifa letu. Wamesema kwamba hatuwezi kuorodhesha shule za kaunti kama vile Wajir sambamba na shule katika kaunti kama Nairobi ama Nakuru. Suala hilo la viwango tofauti ni nyeti na sugu na lazima lishughulikiwe. Ni mojawapo ya sababu ambazo zilitufanya kubuni mfumo wa ugatuzi. Sasa tuna nafasi ya kuhakikisha kwamba shule katika sehemu zote za taifa hili zinapata rasilmali tosha. Ndio sababu tumetenga pesa maalum kwenda katika maeneo ambayo kihistoria yamebaki nyuma, kusahaulika ama hayajapata rasilmali za kutosha. Kwa hivyo, suala hilo lisitutie wasiwasi tena kwa sababu tayari limeshughulikiwa na linaendelea kushughulikiwa. Wabunge kutoka maeneo kama hayo wanastahili kuunga mkono Mswada huu kwa sababu utabuni utaratibu ambao utawezesha shughuli ya kuorodhesha shule kufanywa kwa viwango mbalimbali. Kwa mfano, shule katika kaunti kama Wajir, Tana River ama Kwale zitaorodheshwa kwa njia ya kutufahamisha tujue hali ya kila shule katika maeneo hayo na hali hiyo inachangia vipi matokeo katika shule hiyo. Kwa hivyo, tuorodheshe shule katika kila kaunti ili tujue shule shupavu katika kila kaunti. Tuorodheshe shule katika maeneo, shule za kitaifa na katika viwango vingine vya shule kwa mfano, shule za kaunti ili tujue shule za kiwango cha kaunti ambazo zimefanya mtihani kwa njia bora zaidi. Tuorodheshe shule kwa kiwango cha shule za kitaifa kwa sababu tuna shule za kitaifa katika kila kaunti. Kila kaunti sasa imepata shule ya kitaifa. Tuorodheshe shule katika kiwango hicho cha kitaifa. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}