GET /api/v0.1/hansard/entries/662389/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 662389,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/662389/?format=api",
    "text_counter": 168,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Ababu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 108,
        "legal_name": "Ababu Tawfiq Pius Namwamba",
        "slug": "ababu-namwamba"
    },
    "content": "Kwa hivyo, Mswada huu unatupatia nafasi ya kubuni utaritibu maalum. Hapo mbeleni, shule ziliorodheshwa bila utaratibu. Zimeorodheshwa kiholela. Sheria hii itabuni utaratibu wa kutuwezesha kufanya shughuli hii kwa njia ya utaratibu ambayo ninaamini itazuia udanganyifu. Ni lazima sisi kama Wabunge tuunge mkono hatua hizi hasa hatua ambazo lengo lake ni kuhakikisha kwamba tunaondoa kila aina ya udanganyifu katika mitihani. Ndio sababu nachukua fursa hii kumpongeza Waziri wa Elimu, Bw. Fred Matiang’i, kwa hatua ambazo amechukua kujaribu kuimarisha hali ya wizara na kurejesha heshima katika usimamizi wa mitihani, ingawa sikubaliani naye katika maamuzi yake ya hivi punde ambayo yanaondoa maombi kwa wanafunzi ambao wanajitayarisha kufanya mitihani yao ya mwisho shuleni. Ametangaza kwamba tufutilie mbali wanafunzi kutembelewa na wazazi wao wakati wa muhula wa tatu. Sioni jinsi maombi ya kuombea wanafunzi wanaojitayarisha kufanya mitihani yanavyoweza kuchangia wanafunzi kudanganya katika mitihani. Sioni njia ambayo wanafunzi kutembelewa na wazazi wao inaweza kupelekea udanganyifu katika mitihani. Na ukisema kwamba utafutilia mbali wanafunzi kutembelewa na wazazi wao, je utafanya vipi kwa wale wanafunzi ambao wanasoma kwenye shule ambazo wanarejea nyumbani kila siku? Je, utajenga ukuta wa China kati ya wanafunzi hawa na wazazi wao au na famillia zao? Uamuzi huo wa Bw. Matiang’i ni uamuzi potovu ambao hauwezi kuchangia hata kidogo kuimarisha hali ya mitihani. Ningependa Bw. Matiang’i achukue hatua za kutosha za kuhakikisha kwamba KNEC inasimamia mitihani kwa njia inayostahili. Vile vile, ningependa kuona sheria ikiletwa hapa Bungeni ya---"
}