GET /api/v0.1/hansard/entries/663516/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 663516,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/663516/?format=api",
"text_counter": 19,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Mhe. Spika, pia mimi ningependa kuchangia kuhusu hili jambo la kufariki kwa Mzee Ngala. Mimi kama mtoto wa mwanasiasa ambaye alikuwa anafanya kazi na mzee Ngala kwa hili Bunge, ningependa kutoa rambirambi zangu kama Mbunge wa eneo la Kitutu Chache Kusini. Tena, ningependa kutoa rambirambi zangu kutoka kwa familia yangu ya mzee Dr. Zachary Onyonka, aliyeaga. Mhe. Ngala ni mzee ambaye aliheshimika. Alifanya kazi kama mzalendo na wale Wakenya ambao wako nchi hii wanakumbuka. Vigogo wa zamani walipenda nchi hii, waliamini na walitaka iendelee mbele. Anaheshimika kwa sababu alifanya kazi kama mzalendo. Wakenya wanakumbuka wale vigogo wa zamani kama wazee walioipenda na kuithamini nchi hii. Walitaka nchi hii iendelee mbele. Ningependa kuwaombea wananchi wa Kitui Mungu awabariki kwa kutupa kiongozi ambaye alikuwa anaheshimika. Ni kiongozi ambaye atakumbukwa nchini milele. Ahsante, Mhe. Spika."
}