GET /api/v0.1/hansard/entries/664134/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 664134,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/664134/?format=api",
"text_counter": 297,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "mwingine. Ni lazima wakae wakitega masikio na wajue kwamba ukila kuku, maguu yanaangalia upande wako. Bw. Spika wa Muda, nilimwona Mheshimiwa Junet Mohammed, Mbunge wa Suna Mashariki, akiwa katika hali mbaya sana. Ana shinikizo ya damu ya juu sana. Mkewe alimwomba huyo afisa wa polisi amruhusu ampe dawa lakini alikataa. Ikiwa kitu chochote kitatokea, tutamlaumu nani kama si Serikali? Kwa hivyo, ikiwa itawezekana, Serikali ichukue hatua sasa hivi impe Mheshimiwa Junet Mohammed, Mbunge wa Suna Mashariki, dawa hizo za shinikizo ya damu ili aweze kupona pale ndani. Hatutaki kusikia kitu chochote kimetendeka kwa Mheshimiwa Junet Mohammed kama vile kifo. La mwisho ni kwamba utumishi ni kwa wote bali si kutumikia upande mmoja na kulemea upande mwingine. Bw. Benjamin Kisela lazima aelewe kwamba ni lazima atumikie Wakenya wote pasipo kuegemea upande mmoja."
}