GET /api/v0.1/hansard/entries/664300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 664300,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/664300/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1076,
"legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
"slug": "janet-nangabo-wanyama"
},
"content": "Ahsante sana Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii kuchangia Mswada huu. Ningependa kumshukuru Mhe. Wamunyinyi kwa kuleta Mswada huu. Wakulima wa miwa kutoka upande wa magharibi wanaumia sana. Ushuru hutozwa kwa wale watu ambao wanapeleka sukari viwandani. Sukari kutoka nchi zingine hutozwa ushuru mdogo, lakini wakulima wa humu nchini wanatozwa ushuru mkubwa. Ningependa kuunga mkono wenzangu kuwa ni lazima Serikali inafaa kuwa na mikakati mwafaka kuhakikisha kuwa wakulima wa miwa wamepewa nafasi ya mazao yao, na wapate haki yao kwa wakati unaofaa. Mhe. Naibu Spika wa Muda, Mhe. Chris Wamalwa alisema kuwa kiwanda cha mbolea kinachotarajiwa kufunguliwa Eldoret kifunguliwe haraka ili wakulima wa miwa pia wapate mbolea hiyo. Viwanda kama Nzoia, Butali na Mumias vimeajiri watu wengi ambao hivi sasa wanajimudu kimaisha. Katika kaunti yangu ya Trans Nzoia, wakulima wengi wameacha kupanda mahindi na hivi sasa, wanapanda miwa kwa sababu bei ya mahindi imeenda chini. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}