GET /api/v0.1/hansard/entries/664350/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 664350,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/664350/?format=api",
"text_counter": 139,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wekesa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2742,
"legal_name": "David Wafula Wekesa",
"slug": "david-wafula-wekesa"
},
"content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii ili nami nijiunge na wenzangu kwa kuchangia Mswada huu. Mwanzo, ningependa kutumia nafasi hii kumpongeza na kumshukuru ndugu yangu, Mhe. Wafula Wamunyinyi kwa mawazo ya busara na hekima ya kuuleta Mswada huu. Najua Mhe. Wafula ana ujuzi wa miaka mingi kama mkulima wa miwa na mtetezi wa wakulima wanyonge ambao wamenyanyaswa kwa muda mrefu sana. Tayari, tunajua wakulima wengi wa miwa wamenyanyaswa kwa njia nyingi na hawajiwezi. Wengi wao hawajimudu kununua vifaa vya kupanda na kukuza miwa. Ingekuwa heri kama Serikali ingekuja na mbinu ambazo zitawezesha mkulima wa kawaida kununua vifaa vya miwa kwa bei rahisi na pia kumsaidia apate bei nafuu ya kuuza miwa badala ya kuweka ushuru kwa usafirishaji wa miwa ambao tunajua wazi ni mzigo unaelekezwa kwa wakulima. Mimi najua kuna wakulima wengi ambao tayari wameamua kung’oa miwa kwa ajili ya kupuuzwa na wanyanyasaji ambao wanajinufaisha kwa njia nyingi. Pia najua Serikali ina mipango ya kuleta mbolea ya bei rahisi ili kumwezesha mkulima mdogo kuinunua. Lakini, kusema kweli hiyo mbolea haifikii mkulima wa chini. Wale ambao wanajiweza ndio wanaoinunua kwa wingi na kisha wanamuuzia mkulima kwa bei ghali. Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa hayo machache naunga mkono ndugu yangu."
}