GET /api/v0.1/hansard/entries/666005/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 666005,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/666005/?format=api",
"text_counter": 153,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa hii fursa ili niweze kuchangia Hoja hii. Kabla ya hapo, ningependa kuleta suala la kisheria mbele yako. Kama Wabunge, kifungu cha Saba cha Katiba ya Kenya kinasema kuwa lugha ya taifa ni Kiswahili. Lugha rasmi ya Kenya ni Kiswahili. Unapoangalia Kanuni za Bunge, kifungu cha 77, kinasema kuwa maongezi yote yanayoongewa hapa yaongewe kwa Kiswahili. Sisi tunaoenzi lugha hii tuna matatizo wakati tunafanya utafiti kwa Hoja ambazo zinaletwa mbele yetu. Tumeomba Bunge mara kadha wa kadha itupe Kanuni za Bunge kwa lugha ya Kiswahili ili tuchangie Hoja zinazoletwa hapa Bungeni. Kuzungumza kwa Kiswahili si ujinga. Tunaweza kuzungumza kimombo. Hoja hii ina sehemu mbili. Sehemu moja ni ya wale wanaovamia watu, kuiba na kuua. Sehemu ya pili ni wale walioathiriwa. Hoja hii inazungumzia juu ya wale walioathiriwa. Hoja hii haizungumzii juu ya hatua itakayochukuliwa dhidi ya wale wanaovamia watu. Maana ya hii Hoja ni nini basi? Maana yake ni kwamba sisi kama Bunge tuunge mkono mila ya dhuluma na ushenzi wa wafugaji. Tukitangaza wizi wa mifugo kama janga la kitaifa, Bunge linaunga mkono hatua ya wezi wa mifugo. Mimi najua athari za wizi wa mifugo. Wizi wa mifugo ni mchanganyiko wa jinai kuu zaidi ya kumi. Kuna uuaji, ubakaji, ujeruhi wa watu na wizi wa mali. Najua ni jinai aina kumi lakini kuitangaza kama janga la kitaifa na kuwapa pesa waathiriwa ni kuwaambia wezi waende kesho asubuhi kuiba ng’ombe wengine. Hoja hii haina maana. Inaunga mkono wizi wa mifugo. Ili kama Bunge tulaani hicho kitendo, hii Hoja haistahili kupitishwa. Ni hatari. Tunapoteza lengo. Najua athari. Najua vile watu wameathiriwa. Najua athari ya mtu akikosa mali yake. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}