GET /api/v0.1/hansard/entries/666006/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 666006,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/666006/?format=api",
"text_counter": 154,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Najua vile mtu aliyeuawa anasikia lakini kutangaza wizi wa mifugo janga la kitaifa, ni kupoteza njia. Ningependa kumwambia Mhe. Cheptumo aangalie Uganda iliyokuwa na matatizo kama hayo. Mhe. Museveni alituma jeshi kule. Matatizo haya mengi yamezidi katika eneo la Elemi Triangle katika Bara Afrika. Elemi Triangle inamilikiwa na jamii moja. Ikiwa ni sehemu ya Ethiopia, South Sudan au Kenya, watu wanaoishi Elemi Triangle ni jamii moja. Haya ni masuala ya mila. Mila ya kishenzi; mila ya dhuluma na mila isiyotambua mali wala maisha ya mwanadamu. Tutachukua hatua gani kama Serikali kuhakikisha mila hii ya dhuluma na ushenzi imesimamishwa? Ukisema tuitangaze na tutoe rasilimali tulinde wale watu walioathiriwa, hayo matatizo hayataisha. Kesho asubuhi yataendelea. Mimi kama Mbunge sitaunga mkono sheria yoyote inayoendeleza dhuluma ya maisha ya mwanadamu na unyang’anyaji wa mali. Ukiangalia hii sheria, upande wa pili unaendeleza wizi wa mifugo. Kwa nini Uganda imefaulu kutatua matatizo ya wizi wa mifugo katika eneo la Karamoja? Kwa nini Ethiopia imefaulu? Ni nini kama nchi hatujaweza kushugulikia ipasavyo kuitangaza janga la taifa? Je, kesho asubuhi itazuia wale wavamizi wasiende kuvamia? Hapana. Tunasema tu wale waliovamiwa wapewe pesa na kulipwa fidia lakini wale wanaoenda kudhulumu bado sheria haijachukua hatua juu yao. Kwa hivyo, mimi nimesimama kupinga Hoja hii kwa sababu inaendeleza hiyo dhuluma ya wizi wa mifugo, uuaji wa watu na ubakaji wa wanawake. Lazima tuisimamishe leo; si kesho. Ahsante."
}