GET /api/v0.1/hansard/entries/667149/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 667149,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667149/?format=api",
    "text_counter": 602,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuongeza sauti yangu na kuunga wenzangu mkono. Kuna umuhimu kwa Wakenya kufahamu kuwa mhasibu ni mtu ambaye ana kisomo cha shahada ya juu. Hawa ambao wamepatiwa sheria hii kuwalinda ni manaibu ama wasaidizi wa wahasibu. Hivyo basi, ni muhimu kwa watu kujua tofauti ya aina mbili za wafanyakazi. Wale ambao watakuwa wasaidizi wakitaka kuitwa wahasibu, basi ni sharti warudi vyuo vikuu wakasome kazi ya uhasibu. Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}