GET /api/v0.1/hansard/entries/667243/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 667243,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667243/?format=api",
"text_counter": 696,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Kombe",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 250,
"legal_name": "Harrison Garama Kombe",
"slug": "harrison-kombe"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia fursa hii nichangie Mswada huu. Mswada huu utaondoa utata ambao upo kwa wakati huu. Hazina ya Kitaifa ya Maendeleo ya Maeneo Bunge (NGCDF) inakumbwa na utata. Kwa upande wangu, nilikuwa nimejipanga niitumie kurekebisha barabara mbaya katika Eneo Bunge langu. Barabara hizo zinachukuliwa kwamba ziko chini ya kaunti. Ili kuzirekebisha, ni lazima barua iandikwe kwa kaunti, upewe idhini ndipo uweze kutumia hela za NGCDF kufanya miradi ambayo imegatuliwa. Utata huo utapotea kupitia Mswada huu. Baada ya haya yote kutendeka, ninaisihi Serikali kuu ifikirie barabara za Eneo Bunge la Magarini. Ni jambo la kusikitisha kwamba barabara ya kutoka Sabaki kuelekea Marafa, Baricho hadi Galana, kule ambako kuna shamba kubwa la ekari milioni moja la unyunyizaji maji, kufikia hivi sasa sehemu nyingine hazipitiki kabisa. Ikiwa ni kutumia ng‟ambo ya pili ya mto, pia huo mto wakati mwingine ukifurika kule Galana hakuendeki. Labda watu watumie helikopta ndio wafike maeneo hayo. Kwa hivyo, ni muhimu barabara hii irekebishwe na iinuliwe kiwango chake kufikia daraja la kuwekwa lami. Pia, wakati wa kufanya kazi hii ni muhumu wahandisi wazingatie viwango vya barabara. Tukichukua mfano wa barabara kutoka Malindi kuelekea Lamu, tulifanyiwa ukora maana haikufikia kiwango cha kuitwa barabara ya lami. Iliendelea mpaka ilipofika katika ngazi ama hatua fulani ikakomea pale na tukadanganywa kwamba tumewekewa lami kumbe kwa Kiingereza barabara hiyo ilikuwa imefikia road levelling . Wanakandarasi wakaiachia hapo. Tulipoanza kuitumia haikuchukua hata miezi sita ikaanza kubambuka. Hata hivi The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}