GET /api/v0.1/hansard/entries/667244/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 667244,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667244/?format=api",
    "text_counter": 697,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Kombe",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 250,
        "legal_name": "Harrison Garama Kombe",
        "slug": "harrison-kombe"
    },
    "content": "ninavyozungumza, ukipita Marereni kuelekea mbele ni mashimo tupu. Hivi sasa wameanza kutoka Malindi ndivyo wanaanza kuweka lami yenyewe kuelekea ng‟ambo ya Lamu. Barabara kutoka Mjanaheri kuelekea Ngomeni kuna kituo cha kurushia roketi. Ni kituo kinachostahili kuingiza hela nyingi sana hapa nchini lakini kwa sababu kiko chini ya utawala wa Italia, kituo kile kinapatia hela nchi ya Italia badala ya Kenya. Nchi ya Italia inapata shilingi bilioni 75 kwa mwaka kutoka kwa nchi ya Ufaransa kwa kukitumia kituo kile. Kulingana na marekebisho tuliyoyafanya hapa Bungeni, iwapo kituo hicho kingekuwa kimerudi kwa Serikali, pesa hizo zingeingia hapa nchini na barabara ya Ngomeni pengine ingetengenezwa. Ni matumaini yangu kwamba baada ya Mswada huu kupitishwa, Kamati inayosimamia mipango ya barabara itaweza kuzingatia hayo na kuhakikisha kwamba barabara hiyo inawekwa lami, ama ikizidi ishurutishwe ile kambi ikarekebishe barabara hiyo ya kilomita 11 pekee. Maombi tushafanya. Si hapo tu. Kuna barabara muhimu ambayo inatoka Kibaoni kuelekea Ramada-Adu- Kamale ambako Gavana wa Kilifi Kaunti anatoka. Ni barabara ambayo iko hali mbaya. Wakati wa mvua kama sasa hufurika maji na haipitiki kabisa. Ni matumaini yangu kwamba tulipitisha Hoja hapa Bungeni kwamba kila mwaka kila eneo Bunge litapata kilomita 20 za lami. Hiyo ingetekelezwa ninafikiri kungekuwa na kila sababu hasa kwa watu wa Magarini wapigie kura Serikali ya Jubilee. Lakini iwapo hata inchi moja haitapatikana ninatumai itabidi kujipanga. Katika hayo maeneo, hasa wakati mwingi upigaji kura huja wakati wa mvua na huwa ni shida mpaka utumie helikopta ndio maeneo mengine yafikiwe. Ni kwa nini Serikali isiwajibike na tuupitisha Mswada kwamba kila eneo Bunge lipate kilomita 20 ya lami kwa kila mwaka? Kama jambo hili lingefanyika ninafikiri sasa hivi tungekuwa na kilomita 60, na mwaka ujao tungekamilisha hizo zingine. Kila eneo Bunge lingekuwa na kitu cha kujivunia katika Serikali yetu ya Jubilee. Kwa hakika nina hamu na ningetaka kuendelea, lakini ninaomba nikomee hapo. Ninaunga mkono Mswada huu. Ninatoa nafasi kwa wenzangu wachangie. Asante, Mhe. Naibu Spika wa Muda."
}