GET /api/v0.1/hansard/entries/667253/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 667253,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667253/?format=api",
"text_counter": 706,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Changorok",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1149,
"legal_name": "Regina Nyeris Changorok",
"slug": "regina-nyeris-changorok"
},
"content": "Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda, ningependa kukushukuru kwa kunipatia nafasi hii ili niungane na wenzangu kuunga mkono Mswada huu wa barabara. Barabara ni muhimu katika nchi yetu ya Kenya. Maisha ya mwanadamu yanaenda pamoja na barabara. Ninasema hivyo kwa sababu pasipokuwa na barabara nzuri hata ugonjwa ukitokea watu wengi huangamia. Ninaposema hivi asilimia kubwa ya barabara katika nchi hii ziko katika hali mbaya. Tunapoangalia sehemu nyingi katika Kenya, tunaona kwamba watu wengi hutatizika na hata vyakula kuharibika wakati wa mvua kwa sababu ya barabara mbaya. Unakumbuka kwamba mara nyingine mitihani inachukua muda na inakosa kufanywa siku ile imepangwa kwa sababu ya kutokuwa na barabara nzuri katika sehemu ile. Kuna barabara nyingi huko Pokot lakini ni barabara moja tu ambayo iliwekwa lami kitambo. Hii barabara inachukua sehemu kubwa ya hiyo nchi. Barabara ya Kitale hadi Lodwar, imeharibika sana. Katika Chesegon, wale ambao wamepewa kazi ya kujenga barabara, hawafanyi kazi vile inavyotakikana. Ninataka niseme kwa ukali kidogo kwa sababu barabara hii ambayo imepewa kandarasi juzi ni muhimu. Inaunganisha Kaunti za Pokot, Turkana na Marakwet. Hii barabara inachukua vyakula vingi kutoka Marakwet na Pokot, na hata wananchi kutoka Turkana hutumia barabara hii. Tumesikia kwamba kuna wale ambao wamepewa kandarasi ilhali miezi mingi imepita na kazi haijaanza. Tukiangalia mambo ya daraja, tunakuta kwamba watu wanafariki ng‟ambo nyingine ya mto kwa sababu ya kutokuwa na daraja. Akina mama wengi wamepoteza maisha yao wakati wanajifungua kwa sababu ya barabara mbovu na hawawezi kufikishwa hospitalini. Miezi miwili iliyopita, tulipoteza mwalimu wa Shule ya Msingi ya Lomut kwa sababu hawangeweza kumvukisha mto kwa sababu mvua ilinyesha. Kulikuwa na gari upande huo mwingine wa mto lakini mwalimu alifariki kwa sababu gari halingepita. Ningependa kuungana na wenzangu kwamba ni sharti Serikali itilie mkazo barabara ambazo inasimamia na kuzitengeneza. Ningependa kupongeza Kaunti ya Pokot kwa sababu wametengeneza barabara za mashinani. Jambo hili limesaidia kuimarika kwa usalama wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}