GET /api/v0.1/hansard/entries/667255/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 667255,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/667255/?format=api",
    "text_counter": 708,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Changorok",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1149,
        "legal_name": "Regina Nyeris Changorok",
        "slug": "regina-nyeris-changorok"
    },
    "content": "Serikali ya Jubilee imejaribu na ninatumai tutaendelea kufanya kazi nzuri zaidi kuliko ilivyo sasa. Kule Pokot, tumeahidiwa kutengenezewa barabara tatu na ninaamini kuwa zitatengenezwa kwa muda mfupi ili zisaidia wananchi kusafirisha vyakula vyao. Katika eneo la Pokot Kusini, kuna vyakula vingi haswa maziwa. Maziwa na matunda huharibika kwa urahisi. Barabara inapoharibika na magari yanapokwama, vyakula vyote vinaharibika na jambo hili husababisha hasara na uchumi kuharibika. Wananchi wanaumia kwa sababu wanategemea mapato kusomesha watoto wao. Barabara ni maisha ya wananchi na wasipotengenezewa barabara, nchi haiwezi kusonga mbele. Wananchi hawawezi kufanya biashara kama barabara ni mbaya."
}